TEL: +255 752 920 592

Wajasiriamali, Wakulima Wadogo Tanga Kupewa Mafunzo ya Biashara

Katika kuwainua na kukuza mitaji ya wajasiriamali na wakulima wadogo nchini, Benki ya NBC imeahidi kuendelea kutoa mafunzo ya biashara na kilimo biashara, ili wajasiriamali na wakulima waweze kukuza mitaji yao sambamba na kuendesha shughuli zao kwa ushindani.

Hayo yameelezwa na Meneja Maendeleo ya Biashara wa benki hiyo tawi la Tanga, Aljiran Mbwani wakati akielezea huduma za benki hiyo mbele ya Katibu Tawala Mkoa wa Tanga – Pili Hassani, kwenye maonesho ya nane ya biashara yaliyohitimishwa mwishoni mwa wiki viwanja vya Mwahako jijini Tanga.

Maonesho hayo yalihusisha wadau mbalimbali ikiwemo taasisi za kifedha, mamlaka na taasisi za serikali, wadau wa utalii, wakulima na wajasiriamali kutoka ndani na nje ya jiji hilo.
Mbwani alibainisha kuwa kwa kutambua umuhimu wa wajasiriamali na wakulima jijini humo wamekuwa mstari wa mbele kushirikiana na makundi hayo kwa kutoa mafunzo ya ujasiriamali na kilimo biashara kabla ya kuwapatia mikopo.
“Hata hivyo kwa jiji la Tanga ushirikiano tunaupata zaidi kutoka kwa wakulima wakubwa, hususani wa mazao ya katani na viungo wakati tukiendelea kuwaamsha zaidi wafanyabiashara wadogo na wakulima wadogo. Haya yanafanyika kupitia mafunzo ya biashara kwa wajasiriamali na elimu kuhusu mikopo sahihi tunayoitoa kwa wakulima.’’ alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

About us

Mipango ni app na tovuti iliyojikita katika kutoa elimu ya kifedha na kuwezesha usimamizi bora wa kifedha, binafsi na kufikia malengo ya kimaendeleo.