TEL: +255 752 920 592

Wafanyabiashara nchini kushindanishwa Afrika ili kupata tuzo

Wafanyabiashara nchini wataanza kupatiwa tuzo ili iwe motisha kutanua na kukuza biashara zao ndani nan je ya nchi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Maendeleo na Biashara nchini (TanTrade), Edwin Rutageruka ambaye amezindua tuzo hizo zinazofahamika kama tuzo za chaguo la mteja Afrika ili kuwajengea kujiamini uliofanyika jijini Arusha.

“Wakati tupo Nairobi, Rais Samia Suluhu Hassan alisema anakwenda kufungua nchi yaani watu waje na sisi tutoke. Mmenitia hamasa sana kwa sababu mmefunguka kwenye nchi kama Afrika Kusini, Rwanda na nyinginezo” alisema Rutageruka ambaye pia ni Balozi mteule
“Tanzania tumekuwa kwenye mazingira ya unyonge unyonge hata tukienda katika nchi jirani kama Kenya, Uganda na hata Burundi unaona Watanzania hawajiamini, Trantrade tunasukuma ili wajiamini. Ninyi mmejiamini na mmefunguka na mmesema mnatoka. Cha msingi wafanyabiashara mnatakiwa mjiamini,”

Rutageruka pia ametoa wito kwa kwa waandaji wa tuzo hizo kuhakikisha wanazishirikisha Balozi za Tanzania zilizopo nje ya nchi katika kuhakikisha kuwa Tuzo hizo zinakuwa na tija zaidi kwa biashara ya Tanzania na amewashauri kushirikiana na TanTrade kuangalia uwezekano wa kuhuwisha Tuzo za Rais za Uuzaji wa Bidhaa Nje (Presidential Export Award) ambazo zilikuwepo hapo awali.
Mkurugenzi wa Lavine International Agency na mwasisi wa tuzo hizo, Diana Laizer amesema tayari tuzo hizo zilianza mwaka 2019 na mwaka huu zitafanyika kwa mara ya tatu na sasa wamefungua mlango kwa nchi saba barani Afrika kushikiriki kwa mara ya kwanza.

Na Muandishi Wetu

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

About us

Mipango ni app na tovuti iliyojikita katika kutoa elimu ya kifedha na kuwezesha usimamizi bora wa kifedha, binafsi na kufikia malengo ya kimaendeleo.