TEL: +255 752 920 592

SHINDA UOGA WAKO UJENGE MAISHA YAKO!

 Je ungekuwa huogopi ungefanya nini ili uboreshe maisha yako?  Unataraji hofu na uoga kukupa unachotaka maishani? Je unajua unapaswa ufanye nini ili uweze kushinda hofu na uoga?

Muda sahihi wa kujenga uwezo wa kuvunja mnyonyoro wa hofu na uoga ni sasa, swali ni kwamba unafahamu mambo muhimu ya kuzingatia ili uwe mtu ambaye unajiamini?

Ufanye nini ili uongeze uwezo wa kujiamini na kuwa mtu mwenye kuishi  na uhuru baada kutoka kwenye kifungo cha hofu na uoga?

Mambo yafuatayo ya kuzingatia katika kuongeza uwezo wa kujiamini:-

1. Kuwa na mtazamo chanya na penda kuwa mtu chanya. Mtazamo chanya utakusaidia kushinda mtazamo hasi ambao unazalisha hofu na uoga ndani ya serikali ya akili yako

 2. Zungukwa na watu ambao wanajiamini na wana mitazamo chanya. Hii ni kwasababu ‘wewe’ ni wastani wa marafiki sita unaoshinda nao muda mwingi, hivyo umakini kutambua una marafiki wa aina gani ni jukumu lako

3. Fanya kitu hicho hicho unachoogopa na kuhofia, wewe fanya! Kwasababu kujiamini ni matokeo ya kufanya unachoogopa na kuhofia, kwa kuiambia akili yako unaweza kufanya, mwishowe itaamini inaweza

3. Jiambie kuwa, unataka kujiamini (Self-Talk). Maneno yanaumba …jiambie maneno chanya “Kuanzia Leo sitaki uoga na hofu kutawala maisha yangu”

5. Jifunze kwa kuongeza maarifa. Mara nyingi hofu zinazalishwa na sisi wenyewe pasipo kujua nini tufanye lakini kupitia maarifa inatusaidia kujua.

6. Tafuta Coach, Mentor na  Mwanasaikolojia. Hawa wanakusaidia kujua nini ufanye, kupitia ushauri na programu tofauti tofauti. Baada ya muda unakaa sawa na kujiamini Zaidi

7. Usiishi Leo kwa kufikiria mambo yaliyopita, ishi Leo kwa kujenga kesho yako na sio mambo yaliyopita, kwanza, huwezi badili ya liyopita, Zaidi…ni kudhoofisha kujiamini kwako

John Maxwell mwandishi nguli wa vitabu vya uongozi aliwahi kusema “Binadamu tumezaliwa na hofu ya asili lakini tuna machaguo mawili; hofu kututawala sisi au sisi kuitawala  hofu”.

Bahati mbaya ni kwamba wengi hawajui kuwa akili yako ina uwezo mkubwa kuliko unavyofikiria. Hii ni kwasababu akili ndiko hali ya kujiamini inazaliwa au hofu inakozaliwa msingi wa yote ni aina gani ya mawazo yapo ndani ya akili yako!

Kujiamini ni matokeo ya kuishinda hofu na uoga kwenye maisha yako, jiamini!

Makala imeandikwa na Innocent Ngaoh

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

About us

Mipango ni app na tovuti iliyojikita katika kutoa elimu ya kifedha na kuwezesha usimamizi bora wa kifedha, binafsi na kufikia malengo ya kimaendeleo.