
Serikali Yasema Wawekezaji Wanaongezeka
Serikali ya Tanzania yasema, maombi ya uwekezaji nchini yameongezeka kwa kipindi cha miezi miwili hadi mitatu iliyopita. Hii ni kutokana na wito wa Mheshimiwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwakaribisha wawekezaji wapya na ambao walikimbia.
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Profesa Godius Kahyarara kwenye mkutano na wadau wa uwekezaji ulioandaliwa na Baraza la Taifa la Biashara (TNBC).
Profesa Kahyarara amesema sababu ya mafanikio ni imani waliyojengewa wawekezaji na nchi inapoelekea.
“Maombi ya uwekezaji kituo cha taifa cha uwekezaji (TIC) ni mafuriko, wingi wake haujawahi kutokea. Sasa tunachambua kuangalia uwekezaji wa kimkakati tunaoutaka na hapo tutaeleza idadi ya wawekezaji waliokuja ndani ya muda huu mfupi,” amesema.
Profesa Kahyarara amesema, mbali na wawekezaji wapya kuna wawekezaji ambao walishindwa kukamilisha taratibu ambapo hivi sasa wanawasaidia kukamilisha taratibu hizo, kwani kuna ambao mchakato wao ulikuwa na matatizo na wengine mambo madogo madogo yanayotatulika.
Na Muandishi Wetu
Leave a Reply