Blog

Serikali ya Tanzania Yalipa Madai ya Thamani ya Shilingi 965.1 bilioni

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema hadi kufikia mwezi Aprili mwaka 2021, jumla ya madai yenye jumla ya Shilingi 965.1 bilioni yamehakikiwa na kulipwa.
Hayo yamebainishwa na Waziri Dk Mwigulu wakati akiwasilisha makadiro ya mapato na matumizi ya Wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022.

Dk Mwigulu amesema kwenye kiasi hicho, madai ya wazabuni Shilingi 21.6 bilioni, wakandarasi ni Shilingi 704.5 bilioni, watumishi Shilingi 97 bilioni, madeni mengineyo Shilingi 92.1 bilioni, watoa huduma Shilingi 34.2 bilioni na fidia kwa wananchi wanaopisha utekelezaji wa miradi mbalimbali Shilingi 15.7 bilioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published.