TEL: +255 752 920 592

Riba Benki Isizidi 10%

Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Benki Kuu kuzisimamia Benki zote nchini na Taasisi nyingine ili zipunguze kiwango cha riba kwenye mikopo hadi 10% kushuka chini.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo akiwa Mwanza baada ya kufungua Jengo la BOT>>>>”Mtu anaweza kukopa Milioni 1 na kutakiwa kurejesha milioni 1.5 ndani ya miezi 6 hii ni riba kubwa sana, masharti ya kukopa Bank ni magumu na riba kubwa, naelekeza viwango vya riba vianze kushushwa angalau viwe 10% kwenda chini”

Rais Samia pia amesema Benki zina masharti magumu ambayo yamekuwa changamoto na kuwafanya Watanzania wengi washindwe kukopa Benki na Taasisi nyingine kutokana na masharti ya kukopa kuwa magumu na viwango vya riba kuwa juu.

Rais Samia amesema >>>>”Viwango vya kukopa kwenye Benki ni kati ya 12% hadi 19% Benki Kuu mlifanyie kazi hili, viwango hivi ni vikubwa sana kwa Wananchi wa kawaida”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

About us

Mipango ni app na tovuti iliyojikita katika kutoa elimu ya kifedha na kuwezesha usimamizi bora wa kifedha, binafsi na kufikia malengo ya kimaendeleo.