TEL: +255 752 920 592

Mambo matano (05) ya kufanya ili uwe mshindi kwenye kitu unachofanya

James Clear mwandishi wa Kitabu cha Atomic Habit Alisema “Success is product of your daily habits” akimaanisha kwamba mafanikio ni matokeo ya tabia zako za kila siku, hivyo tabia ina nafasi kubwa ya kukufanya kuwa mshindi au kuwa mtu wa kushindwa.

Ni muhimu kutenga nafasi ya kujifanyia tathimini na kujua tabia zako ni zipi kisha chukua hatua za kujiboresha.

Mambo matano (05) ya kufanya ili uwe mshindi kwenye kitu unachofanya;-

 1. Weka vipaumbele
  Kabla ya kuanza siku nyingine, huwa unapangilia siku yako kujua muda gani utatumia kwenye mambo yenye kuchochea kufanikiwa? Ili uwe mshindi na mwenye ufanisi mkubwa ni lazima uanze kupanga vipaumbele huku kipaumbele muhimu ukianza nacho asubuhi. Ki kawaida, asubuhi mwili huwa na nguvu na akili huwa active kuliko muda wowote katika siku nzima.
 2. Tarajia tofauti unavyodhani.
  Kuwa na matarajio ya ushindi kwenye maisha sio vibaya lakini kosa ni kuweka matarajio pasipo kukumbuka, kati kati ya safari changamoto ni lazima, kuanguka ni lazima, kufeli ni lazima, kupanda na kushuka ni lazima. Hivyo, ni muhimu kutarajia changamoto ili usikate tamaa matarajio yanapoenda tofauti na uhalisia wa maisha yenyewe na hatimae kuvunjika moyo. Kuzuia kuvunjika moyo kwa matarajio unayoweka, anza kutarajia changamoto na kujiandaa kiakili kuyakabili hadi ufikie mafanikio.
 3. Ongeza kasi ya kujifunza kupitia kufeli kwako au kushindwa kwako
  Je, ukifeli ndio unakata tamaa na kuacha kupambana tena? Kumbuka, kukata tamaa haifanyi maisha kuwa rahisi, unapofeli ni nafasi yako kujifunza kupitia kufeli kwako na makosa yako ili ujue nini ufanye uweze kupata matokeo mazuri kwenye yale unayofanya baadae. usikate tamaa, haijalishi umefeli mara ngapi na umekosea mara ngapi muhimu jifunze kisha chukua hatua na kusonga mbele.
 4. Kuwa na muendelezo na kitu unachofanya
  Unapokutana na vikwazo usikubali kughairi hata siku moja, endelea kufanyakazi, iwe unajisikia au hujisikii. Fanya jambo moja mpaka mwisho ndio siri ya ushindi ilipojificha, usiishie njiani Ushindi upo mwisho wa safari. Kuna msemo maarufu wa wachina unaosema “Hatua elfu moja huanza na hatua moja”.
 5. Kuwa na mtazamo chanya
  Usiogope kufeli wala kukosea kuwa na mtazamo chanya kwa maana, kukosea kupo kufeli kupo na kumbuka Ushindi ni mchakato. Ndani ya mchakato kuna vikwazo, changamoto, matatizo hivyo isikutatishe tamaa ya kuendelea, bali iwe chachu ya kuendelea kusonga mbele kwenye kitu unachofanya. Mtazamo chanya utajengwa kwa kuongeza maarifa, kwa kusoma vitabu, kuhudhuria semina, kusikiliza video za hamasa youtube, kusikiliza audio books pamoja na Podcast mwisho kabisa kufuatilia makala mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii. Pia kuzungukwa na marafiki wanaokupa moyo na maneno ya ushindi.

Baada ya kuona nini ufanye Ili uweze kuwa mshindi, ni lazima ujenge mfumo wa ushindi ambao utakusaidia kupata ushindi kwenye kitu unachofanya; unajiuliza mfumo wa Ushindi ni nini?.

Mfumo wa ushindi, ni mikakati ambayo unapanga ili ujue utafanya nini ili uweze kupita kwenye mchakato wenyewe, marafiki wanao kuzunguka ili upate ushauri na mazingira sahihi hasa wakati wa changamoto, kujielimisha kila wakati.

Kumbuka wewe ni mshindi

Wakati ndio sasa, thubutu, kisha fanyia kazi haya uliyojifunza, utapata Ushindi na matokeo makubwa kwenye kitu unachofanya

Nakutakia utekelezaji mwema.

Na muandishi wetu

Comments

 • Baraka Range

  Unamafundisho mazuri sana ndugu, hongera. Lakini pia nahitaji niwe jaribu sana na wewe nahitaji kujifunza mengi na kujiimarisha katika kipindi hiki Cha ujana.

 • Allison

  My brother recommenmded I woluld possibly lioe this website. He used to be entirelyy right. Thhis put up treuly madde mmy day. You cann't imagtine just how much tine I hhad spent ffor this information! Thank you!

 • Alma

  Whyy visitorrs still use too read newss papeds when in this technologocal globe everyting is availazble onn net?

 • Del

  Touche. Outstanding arguments. Keep upp the great spirit.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

About us

Mipango ni app na tovuti iliyojikita katika kutoa elimu ya kifedha na kuwezesha usimamizi bora wa kifedha, binafsi na kufikia malengo ya kimaendeleo.