TEL: +255 752 920 592

KUTANA NA TRIVIN FARM, KIJANA ANAYELIMA PILIPILI NA KUUZA KATIKA SOKO LA UINGEREZA

Nchini Tanzania, Sekta ya Kilimo ni muhimili wa maendeleo ya uchumi. Sekta hii inachangia kiasi cha nusu ya pato la Taifa , robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na chanzo cha chakula pamoja na utoaji wa fursa za ajira kwa zaidi ya 75% ya Watanzania. Katika harakati za kuunga mkono kauli mbiu ya Tanzania ya Viwanda kutana na Mtanzania, Mkulima wa Pilipili anayehudumia soko la kimataifa.

 Kijana Vincent Paschal Zawadi mwenye umri wa miaka 30 alianza biashara ya kilimo mwaka 2014. Vincent ana stashahada ya masomo ya Sinema na Televisheni aliyo hitimu mwaka 2015. Katika tabia yake ya kupenda kutembelea taasisi mbalimbali na kutafuta fursa zitakazo mfaa, Vincent aliona fursa kwenye kilimo cha pilipili baada ya kutembelea taasisi ya TANTRADE ambayo majukumu yake ni pamoja na kusimamia na kuendeleza mikakati ya biashara nchini, kusimamia na kuendesha soko la ndani, kushirikiana na taasisi nyingine katika kuzalisha bidhaa na kutoa huduma, kuijengea uwezo jumuiya ya wafanya biashara, kuandaa maonyesho ya biashara na mengine mengi. Kupitia TANTRADE, Vincent alipata fursa ya kushiriki maonyesho mbalimbali na kukutana na wateja wa bidhaa zake moja kwa moja.

Katika kuanzisha kampuni ya Trivin Farm, Vincent aliamua kuendesha biashara yake kwa kutumia njia za kisasa, vilevile aliepuka gharama kubwa ya kununua mashamba kwa kuamua kukodi mashamba kutoka kwa wakulima vijijini.

Baada ya kuingia kwenye biashara ya kilimo, Vincent aliona ugumu uliopo kwenye biashara ya kilimo hadi kufanikiwa, hii ikiwa kuanzia kulima hadi kuuza mazao ndani ya nchi. Changamoto za soko la ndani ya nchi kama bei kuwa ndogo na madalali kuwa wasumbufu sana, ilipelekea kutafuta masoko mengine nje ya nchi ndipo kuanza kuuza bidhaa zake katika soko la Uingereza.

Alipoulizwa ni kwa nini ameamua kufanya kilimo na si ajira aliyosomea, Vincent alijibu “Napenda sana kilimo, nimekulia katika familia ya mkulima, ndio maana napenda na kuamini sana katika kilimo!”

Kama ilivyo kwa mfanya biashara yoyote, Vincent pia amekutana na changamoto mbalimbali zilizompa hasara mara kadhaa mfano mzigo kukataliwa pindi ufikapo kwa mteja kutokana na kutofikia ubora unaotakiwa. “Tofauti na zamani, Kwa sasa tumeshajua jinsi ya kufikia viwango vya ubora wa pilipili unaotakiwa, ila kabla ya hapo tulipoteza mizigo zaidi ya mara sita.  Pamoja na kulipa faini ya kutelekeza mzigo baada ya kukataliwa, Ila hatukukata tamaa!”

Baada ya kuvuna na kuchambua pilipili zenye ubora wa soko la nje, TRIVIN huzipaki pilipili hizo kwenye mabox maalum kisha kusafirisha kwa ndege kwenda kwa wateja wake.

Ushauri wa Vincent kwa vijana wanaotamani kufanya biashara ya kilimo ni “Kijana asiogope kilimo, aingie ila asitegemee mafanikio ya haraka! Chanagamoto ni nyingi sana, ila kikubwa ni kuwa na ndoto kubwa (vision), na kila kitu kitaenda sawa.” Pamoja na upeo, Vincent anashauri kabla ya kuanza biashara husika, vijana wafanye utafiti kuhakiki kama soko la bidhaa husika lipo au la. Pia wajitahidi kuongeza thamani kwenye mazao wanayolima ili kuwa na uhakika wa ubora wa mazao yao yafikapo sokoni ili kuepuka hasara.                       

 Pamoja na kilimo cha pilipili, —–pia wanafanya kilimo cha vitunguu, bamia, nyanya chungu na nyanya na kuuzia soko la ndani ya nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

About us

Mipango ni app na tovuti iliyojikita katika kutoa elimu ya kifedha na kuwezesha usimamizi bora wa kifedha, binafsi na kufikia malengo ya kimaendeleo.