TEL: +255 752 920 592

Kutafuta pesa ni ngumu, Ila umewahi Kujaribu kutunza pesa? Ni ngumu zaidi.

Wengi tunafahamu juu ya ugumu wa kutafuta fedha, ni jambo ambalo tunaliskia nyumbani, shuleni, mitaani, kwenye hadithi, nyimbo nk.

 

Lakini mara chache tunasikia juu ya ugumu wa kutunza fedha, niwazi kwamba watu wengi hupata
fedha lakini wachache sana wana hudumu nazo, iwe katika ngazi ya familia, mtaa ama mji watu
wenye pesa nyingi niwa chache sana.

 

Fedha nikama sumaku, unapoipata huvuta mambo mengi sana, hapo inahitaji kuwa na busara wa
hali ya juu kuweza kuhimili vyote vinavyo fuata. Niwazi pesa ya weza kuvuta ulevi, wapenzi, marafiki, shopping au ajali. Fedha pia huvuta umaskini kwa sababu inakupeleka kwenye kuzimaliza na sio kuzizalisha.

 

Biashara nyingi zenye mtaaji zimekufa, wastaafu wengi wamefilisika, wachimbaji wengi mamilioni
yamepita mikononi mwao, nakadhalika.

Kusema haya ni muhimu kwanza kuyakubali;
Kutunza fedha ni kitu kigumu sana,
Kuwa na fedha ni mtego, na nirahisi kujitega,
Kwa maana hii kutunza fedha ni ujuzi na ni lazima kujifunza, ni utamaduni lazima kuujenga, kwa mtu binafsi au familia.

 

Kwa uzoefu wangu haya ni mambo ya kutafakari

  1. Wengi wetu hatuna kiwango cha kuhifadhi katika kila pesa tuipatayo, muhimu kuwa na
    kiwango ulichojiwekea cha kuhifadhi. Kuna jamii ambazo kwao kiwango ni 30%,
  2. Dharura hutokea bila taarifa na humaliza akiba, muhimu kuwa na savings kwa ajili hiyo, ama
    kuwa na vitu kama bima,
  3. Akiba isiyo na malengo ni rahisi kutumika, lakini yenye malengo sio rahisi kutumika na pia ni
    rahisi kufikika,
  4. Chukua kalamu na karatasi andika kuanzia siku saba zilizopita ni vitu gani visivyo vya muhimu
    umevinunua, basi kuanzia kesho anza kuvigeuza hivyo kuwa akiba,
  5. Fedha ndogo ni rahisi kuitumia vibaya kwa sababu haina maumivu lakini ndio wengi
    tunaipata mara kwa mara, anza kujifunza kuweka akiba ya fedha ndogo,
  6. Tukijifunza kutunza kumbukumbu ya matumizi yetu tutajifunza kitu juu ya mwenendo wa
    upatikanaji na utumiaji wa kipato chetu.

Kuandika ni mwanzo wa kufikiri tuanze hapo

Haya ni mawazo yaliyo nijia juu ya mada hii, asanteni sana natumaini na nyie mtaendelea kutafakari Zaidi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

About us

Mipango ni app na tovuti iliyojikita katika kutoa elimu ya kifedha na kuwezesha usimamizi bora wa kifedha, binafsi na kufikia malengo ya kimaendeleo.