
Bei Ya Petroli Yapanda
Mwandishi Wetu
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (Ewura) imetangaza bei kikomo za mafuta ya petroli kwa mwezi Juni ambapo imezidi kuongezeka kwa mkoa wa Dar es Salaam kulinganisha na Mei, 2021.
Kwa mwezi Juni bei ya rejareja ya petroli imeongezeka kwa Shilingi 80 kwa lita na dizeli dizeli Shilingi 34.
“Petroli itauzwa Shilingi 2,249 na dizeli Shilingi 2,073 na mafuta ya taa Shilingi 1,957 kwa lita” imeeleza taarifa hiyo.
Taarifa ya Ewura imeeleza bei hizo zimepanda kwa mikoa ya kaskazini inayojumuisha Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara ambapo bei zimeongezeka kwa Shilingi 69 petroli, dizeli imepungua kwa Shilingi 116.
Kadhalika bei mpya haitaathiri mikoa ya kusini ambayo ni Lindi, Mtwara na Ruvuma kwasababu wataendelea na bei za mwezi Mei kwa kwakuwa hakuna shehena iliyopokelewa kwenye bandari ya Mtwara.
Leave a Reply